Kazi za Uwezo na Twaweza zinafadhiliwa na wafadhili makini na wapenda maendeleo, ambao ni pamoja na:

Mfuko wa William na Flora Hewlett
Mfuko wa William na Flora Hewlett umekuwa ukitoa misaada tangu 1967 ili kutatua matatizo ya kijamii na kimazingira ya ndani ya nchi yao na duniani kote.

Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Uingereza (DFID)
Hii ni Idara ndani yaSerikali ya Uingereza yenye jukumu la kusaidia kukuza maendeleo na kupunguza umaskini.

Shirikala Kimataifa la Maendeleo la Sweden (SIDA)
Sida ni shirika la kiserikali lililo chini ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Sweden, linalosimamia misaada ya maendeleo ya nchi za nje.

Hivos
Hivos (Taasisi ya Ushirikiano wa Maendeleo ya Uholazi) ni shirika la maendeleo la Kiholanzi linaloongozwa kwa misingi na maadili ya utu.

Benki ya Dunia
Benki ya Dunia ni chanzo muhimu cha msaada wa kifedha na kiufundi kwa nchi zinazoendelea duniani kote.

Mfuko wa Fedha wa Uwekezaji wa Watoto (The children’s Investment Fund Foundation)
Mfuko wa Fedha wa Uwekezaji wa Kuhudumia Watoto unalenga kudhihirisha kwa vitendo kuboresha maisha ya watoto wanaoishi katika dimbwi la umaskini katika nchi zinazoendelea.